Mahakama imetoa amri kwa Rais Kenyatta kuzuia kuchapishwa kwa sababu za kutowateua Majaji sita aliokosa kuwateua.
Mahakama pia imetoa amri kusitisha uchunguzi wowote wa majaji hao. Hii ni baada ya tume inayosimamia Mahakama kutaka Rais awape sababu za mbona Majaji hao hawakuteuliwa.
Tume ya inayosimamia Idara ya Mahakama [JSC] pia imezuiliwa kuwachukulia hatua yoyote au uchunguzi majaji hao.
Akitoa maelekezo hayo, Hakimu Jastus Makau amesema kuwa maelekezo hayo yanafaa kufuatwa na kutekelezwa ipaswavyo.
Kulingana na kipengele cha miamoja sitini na sita cha katiba, Rais Kenyatta alipaswa kuwateua majaji wote waliopendekezwa na Tume inayosimammia Mahakama. Rais alikosa kuwateua akisema kuwa wana dosari.
Amri hii imetolewa baada ya Benard Okello kuelekea mahakamani akitaka Majaji waliokosa kuteuliwa na Rais kuteuliwa kuingana na katiba inavyosema.