• Mon. May 13th, 2024

Mwanafunzi Wa Kidato Cha Nne Auawa Kwa Kudungwa Kisu Bomet

Oct 11, 2021
493 300

Mwanafunzi wa Kidato Cha nne katika Kata ndogo ya Siorongoi, Cheplingu kaunti ya Bomet ameuawa kwa kudungwa kisu.


Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 24 anadaiwa kudungwa kisu mara mbili kwenye shingo baada ya kujibizana na mwanamke ambaye alikuwa mgeni katika eneo hilo.


“Alama hizi za kujeruhiwa zinaonyesha marehemu alidungwa na kisu. Damu ilimwagika mahali pote na hata matone mengine yameonekana katika kituo Cha Afya Cha Siorongoi ambapo alikuwa amekimbizwa na msamaria Mwema,” alisema Chifu wa Siorongoi Bwana Joseph Ngeno.


Mwanamke huyo anayedaiwa kutekeleza unyama huo alitoroka baada ya tukio hilo. Aidha mwanamke huyo alikuwa amehamia eneo hilo kutoka Sotik.


Imebainika Marehemu alikuwa mwanafunzi wa Kidato Cha nne katika Shule ya Upili ya Kapsinendet katika eneo bunge la Chepalungu.


Maafisa wa Polisi wanamzuilia Mshukiwa mmoja wa kiume atayesaidia katika uchunguzi.
Bwana Nelson Masai ambaye ndiye afisa mkuu katika Kituo Cha polisi ya Kaunti ndogo ya Chepalungu amesema Maafisa wapo katika eneo hilo ili kuendelea na uchunguzi.


Mwili wa Marehemu umelazwa katika makafani ya hospitali ya Rufaa ya Longisa.

READ ALSO: Jaribio la Kujitoa Uhai Latibuka Baada ya Mshukiwa Kumuua Mke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *