• Sat. Apr 27th, 2024

Kivumbi Kagure Kuwania Ugavana Nairobi Mwaka wa 2022

Nov 26, 2021
482 300

Mwanabiashara shupavu katika jiji la  Nairobi Agnes Kagure sasa ametangaza wazi kuwa atawania kiti cha ugavana Nairobi mwaka ujao.

Kagure ametangaza hii leo katika mkutano wa Azimio la Umoja kule kaunti ya Nyeri mbele ya  umati na wazee wa jamii ya Agikuyu.

Kagure  alikua amendamana na kiongozi wa ODM Raila Odinga pamoja na mama Idah Odinga wakati wa hafla hiyo.

Sasa anaungana na Tim Wanyonyi pamoja  na Margret Wanjiru katika kinyanganyiro hicho  cha  ugavana Nairobi.

Bado hajaweka wazi kuwa atawania kiti hicho kupitia chama gani japo kuna fununu kuwa huenda akaingia ndani ya chama cha ODM.

‘‘Kwa wakenya wote sisi tuko salama kwa mkono wa baba kama rais wetu lakini Mlima Kenya  iko salama mkononi mwa Agnes Kagure kama gavana  na hivi karibu nitazindua rasmi azma yangu ya ugavana.’’ Kagure alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *