• Mon. May 20th, 2024

Jamii ya Waluhya Waombwa kuungana

May 25, 2021
414 300

Wananchi katika eneo la Kalenda eneo Bunge la Malava wameombwa kushirikiana na Uongozi wa Kaunti Ndogo ili kuhakikisha mahitaji yao yanashughulikiwa ipaswavyo.

Wakizungumza katika Mazishi eneo Hilo, Mbunge wa Malava Mheshimiwa Malulu Injendi na Mwakilishi wodi wa Shirungu wameahidi kuhakikisha maswala ya miwa ya wakulima wadogo yanashughulikiwa ili wapate faida kutokana na upanzi wa miwa.

Aidha, Mheshimiwa Malulu ameongeza kuwa jinsi alivyoinua masomo katika eneo hilo na wanafunzi kuanza kupita Mitihani yao hivyo ndivyo atakavyofanya maswala ya Miwa. Pia amewataka wanajamii ya Mulembe kuungana ili kuhakikisha kuwa Mheshimiwa Musalia Mudavadi anapita kura mwaka wa 2022.

“Nimeamua kurudi nyumbani sasa. Nawaomba tuweze kuungana ili kuhakikisha kuwa mwaka ujao Mwenzetu Musalia Mudavadi aweze kupita kura mwaka ujao. Hata kama ataanguka tuanguke pamoja. Wakati mwingi tumesimama na Baba(Raila Odinga)lakini ametuangusha. Sasa tusimame na Mwenzetu ili tutwae uongozi.”

Pia Mheshimiwa Injendi amewaomba wananchi wa eneo Bunge la Malava kuweza kumregesha uongozini kwa Muhula mwingine ili atimilize miradi ambayo alianzisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *