• Wed. May 8th, 2024

Jamaa Afariki baada ya Kujirusha Kwenye Daraja la Kilifi

Aug 7, 2023
292 300

Mwili wa mwanamume mwenye umri wa makamo umepatikana baharini, baada ya jamaa huyo kudaiwa kujirusha kutoka kwenye daraja la Kilifi jioni ya jana

Kulingana na maafisa wa polisi waliopata taarifa kutoka kwa kitengo cha usalama wa baharini, jamaa huyo alipatikana akiwa amefariki, baada ya kujitupa kutoka juu ya daraja hilo, na kisha kugonga mawe kabla ya viungo vyake kadhaa kuvunjika na kufariki papo hapo

Akithibitisha kisa hicho Esther Mwendwa, ambaye ni naibu kamanda wa polisi eneo bunge la Kilifi Kaskazini ameeleza kuwa, mwili wa jamaa huyo ambaye haujatambulika kufikia sasa, unaendelea kuhifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Rufaa ya Kilifi

PHOTOS: Padme initiative-Kilifi Chapter

Kamanda huyo aidha amewataka wananchi kuchukua hatua za kutafuta ushauri nasaha, endapo yeyote ametatizikia kiakili, haswa wakati huu mgumu wa maisha, ili kuzuia visa kama hivi kutendeka

Polisi wameanzisha uchunguzi kutambua kiini cha kisa hicho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *