• Sat. Apr 27th, 2024

Humanitarian Network Wahimiza Serikali Kutatua Hali ya Ukame Nchini

Nov 11, 2021
346 300

Serikali  imetakiwa kuangazia Kwa undani swala la ukame katika kaunti  23 zilizoathrika na hali ya ukame nchini watu milioni 2.5 wakiathrika.

Kulingana na Jane Wariwe kutoka Samburu Women Trust chini ya mwavuli wa ASAL Humanitarian Network (AHN)  ametaka serikali kushirikisha  jamii zilizoathrika katika programu kama vile ununuzi wa mifugo Yao ama nyama na tume Kenya meet Commission ,msaada wa vyakula na hata usambazaji wa raslimali muhimu zinazofanya jamii kuzozana maeneo hayo.

‘‘Kwa sasa wengi wameathirika na itakuwa vigumu hali ikiendelea kuwa hivi.Kina mama wetu na watoto wameathirika zaidi kwani ukosefu wa chakula,vituo vya afya hatuwezi fika  na hata lishe kwa mifugo ni  shida.’’ Jane alisema

Hali ya Ukame katika kaunti za ASAL PICHA/MAKTABA

Jane anasema kuwa wengi wa kina mama na watoto wameathirika na wameshindwa kabisa kupata huduma za Afya,na hata vyakula haswa wale wajawazito.

Wametaka serikali Za kaunti pia kushirikisha wenyeji katika kaunti hizo katika mazungumzo    Ili waweze kuimarisha usalama Kwani wengi wanapigania raslimali kama vile maji na mahali pa kulisha mifugo.

‘‘Serikali za kaunti ziwe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanashirikisha jamii katika mpango mzima wa kuhakikisha kuwa ukame na baa la njaa hauleti vurugu baina yao.’’ Aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *