• Sat. Apr 27th, 2024

Gavana Lenku Aongoza Maelfu Kupigia Debe Azimio Kajiado

Feb 18, 2022
456 300

Msemaji wa jamii ya Maa ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Kajiado ameongoza maelfu katika siasa za Azimio kaunti hiyo akiwataka wa Masaai kumpigia kura kinara wa ODM Raila Odinga.

Lenku amemtaja Raila Odinga kama Mwaniaji Bora wa urais na kwamba ni wakati wa kumuunga mkono katika harakati hizo ili jamii hiyo iweze kuwa ndani ya serikali ijayo.

Aidhaa ametaka jamii kutogawanyika kupitia vyama kwani ndani Azimio watakuwa na Umoja.

‘‘Nataka sisi wote tuingie ndani ya Azimio la Umoja,Kinara wa ODM Raila Odinga ndiye yuko na uwezo sasa kuongoza,na Azimo linatuleta pamoja kama jamii…wale ambao bado wako nje meli iko karibu kuondoka tujitokeze.’’ Lenku alisema.

Alikuwa anazungumza baada ya kuzindua rasmi daraja la Paai Kule Kajiado East.

Daraja Hilo limekuwa kikwazo kikubwa Kwa wakaazi kwani hawakuwa na popote Kupitia haswa wakati wa mvua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *