Ukosefu wa sodo umeendelea kuwa changamoto kubwa miongoni mwa watoto wasichana na ipo haja ya hatua za haraka kuchukuliwa.
Hii ni kulingana na Afisa mkuu wa Baraza la vijana NYS Roy Sasaka Telewa.
Kulingana na Telewa amekuwa akishirikiana na makundi ya vijana kusaidia watoto hao.Hii leo Baraza hilo lilipokea sodo elfu tatu kutoka kwa wakili George Gathuki
READ ALSO: Vulnerable youth to benefit from 34,095 Masks donation
“Tumekuwa tukishirikiana na makundi ya vijana na washirika mbali mbali kutathmini shida ya vijana na hata watoto kwa lengo la kuja na jibu kwa changamoto hizi na ndio maana tumepokea sodo paketi elfu tatu ambazo tutasambaza.” Roy alisema.
Gathuki kwa upande wake amedokeza kuwa amekuwa akipokea usaidizi kutoka kwa marafiki wake mtandao wa facebook.
“Nimeongea na marafiki na walikua wakichanga chini ya mpango wa wezesha dada na tukapata usaidizi huu..na tutaendelea na mradi ili tuweze kusaidia wasichana wengi zaidi.” George alidokeza.