• Mon. May 6th, 2024

Shirika La Nubian Rights Forum Lalamikia Ucheleweshaji Wa Rufaa Ya Huduma Namba

Nov 8, 2021
197 300

Shirika La Kutetea haki la Nubian Rights Forum Limemwandikia Rais wa Mahakama ya Rufaa Hakimu Musinga likitaka kupewa tarehe ya Kusikiliza kwa rufaa yao juu ya ubaguzi katika kupeanwa kwa Huduma Namba.


Mwaka 2019, Shirika hilo kupitia wakili wao lili kata rufaa kuhusiana na ubaguzi katika kupeana Huduma Namba.


Kufikia sasa, zaidi ya mwaka mmoja hawajapewa tarehe ilhali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amekata rufaa baada ya Uamuzi kutolewa tarehe kumi na nne Oktoba mwaka huu kuwa hapakuwa na Ulinzi wa Data katika kupeana kwa Kadi za Huduma Namba na tayari ashapewa tarehe ya Kusikizwa kwa kesi yake.


Wameishutumu idara ya Mahakama kwa kutoa tarehe hizo kwa ubaguzi na kutojali maslahi ya wananchi.
Akizungumza baara ya kupeana barua hiyo, Mwenyekiti wa Shirika hilo, Shafi Ali Hussein amesema kuwa ni hujuma kesi yao kutosikizwa na Mwansheria Mkuu ashapewa tarehe ya kusikizwa.


“Tulileta kesi ya Huduma Namba 2019 na Kesi hiyo ilipoisha, tulikata Rufaa na Mpaka leo hatujasikizwa na hatujapewa tarehe hata ya kusikizwa kwa kesi yenyewe. Kesi ya Katiba Institute ilipoamuliwa, Mwanasheria Mkuu amekata rufaa na tayari ashapewa tarehe ya kusikizwa. Kuna haki kweli iwapo mahakama inakandamiza haki zetu kwa kuipa serikaloi nafasi ya mbele na ni sisi tuliotangulia? Hii ni hujuma kwa kuwa kesi ya mwanasheria mkuu ikisikizwa kabla ya yetu, hapatakuwa na haki,” Alisema Shafi.


Adiha ameahidi kuja na jamii nzima ya Wanubi katika mahakama iwapo kesi ya Mwanasheria Mkuu itasikizwa kabla yao.

READ ALSO:Nubian Community Vows To Be Unshaken Out Of Their Ancestral Land of AL Aqsa Mosque


“Nitawatoa wanubii wote katika nyumba zao tuje hapa nje ya mahakama iwapo, kesi ya Mwanasheria Mkuu itasikizwa kabla ya yetu.,” aliongeza Shafi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *