• Thu. Sep 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Nubian Rights Forum latishia kuishtaki serikali kwa ubomozi wa makaazi

May 11, 2021
317 300

Antynet Ford

Shirika la kutetea haki la Nubian Rights Forum limeitaka serikali kuwajibika na kuwasaidia wananchi ambao nyumba zao zilibomolewa na shirika la reli katika maeneo ya Kibos na Soweto katika kaunti ndogo ya Kibera Jijini Nairobi.

Akizungumza hii Leo, mwenye kiti wa shirika hili, Bwana Shafi Ali Hussein amesema kuwa bomoa, bomoa ambazo zimekuwa zikifanyika katika maeneo ya Nakuru, Njiru, Mishomoroni na maeneo mengine ya hivi punde ikiwa ni Soweto katika eneo la Kibera ni kinyume cha sheria.

Amesema hili ni kwa sababu maagizo ya koti huwa hayatiliwi maanani na bomozi zenyewe hutukia nyakati za usiku na kuwaacha wakaazi kwenye baridi wasijue pakuenda.

Aidha amesema kuwa kesi dhidi ya serikali, Shirika la huduma la jiji la Nairobi (NMS) na kaunti ya Nairobi itapelekwa kotini juma lijalo ili wananchi wapewe haki. Wanaharakati hawa wanaitaka serikali iwajibike na kuwasaidia wananchi hawa wanaofaa kulindwa na katiba.

“Tunataka kuambia Rais Uhuru Kenyatta maana tumemchagua, wanafaa kuwajibika kwa kuwa hawa wakenya wanaopata shida hizi zote wana haki na wanafaa kupewa makaazi, maji safi na huduma za afya,” alisema Bwana Shafi.

Pia kesi ya bomozi za kule Kibos Kisumu itaanza kusikizwa kesho.  Wameitaka serikali kutoingilia au kwenda mahakamani na kuwashawishi majaji ili wananchi wapewe haki yao.

“na waache hiyo mtindo ya kuvunjia watu nyumba halafu wanaenda kotini kuhitilafiana na na mahakama na majaji ili kesi zisikizwe kwa faida yao. Sisi tunaomba mahakama ifanyie haki hawa maskini, hawa ni wakenya na wazalendo wanaopiga kura,” aliongeza.

Aidha wameitaka serikali iwajibike na kuwapa haki wananchi hawa kwa kuwa ardhi hizi walizotimuliwa kutoka kwazo ni zao kisheria, na pia wanahangaika msimu huu wa mvua na wanaweza kushikwa na maradhi kama vile virusi vya Korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *