610 300
Mwanamke mmoja amekimbia nyumba yake huko Bondo, kaunti ndogo ya Siaya baada ya kuchomwa na uji moto na mumewe kufuatia ugomvi wa kinyumbani.
Immaculate Akoth, 19, anasema amepata majeraha ya moto na bado hajapata huduma za afya kutokana na kushindwa kumudu ada za hospitali.
Akoth ambaye ni mama wa mtoto mmoja ametoroka Bondo na kupelekwa kaunti ya Homabay anasema mumewe ambaye ni mvuvi alirudi usiku na kuanza kugombana.
Anasema mume huyo aliyekasirika alienda kuchukua uji uliokuwa ukitokota jikoni na kummwagia.
Akoth ana majeraha ya moto kwenye sehemu ya juu ya mwili wake na sasa anatafuta haki baada ya kuripoti kisa hicho jana katika kituo kikuu cha polisi cha Kisumu.