• Fri. Apr 19th, 2024

Havi Ajiunga na UDA Kuwania Ubunge Westlands

Nov 22, 2021
287 300

Mwenyekiti wa Chama cha LSK Nelson Havi  amekihama rasmi chama cha ANC na kuingia chama cha naibu rais cha UDA.

Kulingana na Havi anataka kutumikia wakaazi wa Westlands Bungeni akiwa katika serikali akionesha imani kuwa UDA utashinda uchaguzi mkuu.

Havi amepokolewa rasmi na naibu rais William Ruto kule Karen hapa Nairobi.

‘‘Ni kweli nimeingia katika chama cha UDA nataka nitumikie wakaazi wa Westlands nikiwa kwenye serikali na tuko na imani kuwa chama cha UDA kupitia naibu rais William Ruto kitaunda serikali mwaka ujao.’’ alisema

Havi ameapa kuimarisha miundo Msingi ,na utunzi bora wa Sheria zinazonufaisha wakaazi wa Westlands na wakenya kwa Jumla.

‘‘Katika manifesto yangu nimeweka wazi kuwa nitasaidia katika utunzi wa sheria bora,nitahakikisha kuwa watu wa Westalnds wanapata mgao mkubwa kutoka serikali kuu na mwisho   nitahakikisha kuwa barabara,shule zote zimejengwa.’’ Havi alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *