• Fri. May 3rd, 2024

MCA Doris Kanario Ataka Ushuru wa Miraa Kuondolewa na Kaunti ya Nairobi

Oct 19, 2021
688 300

Viongozi kutoka jamii ya Ameru hapa Nairobi sasa wanataka serikali ya kaunti ya Nairobi kufuata nyayo za gavana wa Mombasa Hassan Joho ya kuondoa ushuru katika mmea wa miraa.

Wakiongozwa na  Doris Kanario wanasema kuwa wafanyibiashara wengi wa miraa bado wanahangaika jijini na maswala ya ushuru.

Pia wansema kuwa hawana soko la miraa Nairobi huku akipeana mfano wa mtaa wa Carlifonia,Majengo na Eastleigh.

‘‘Tunataka ushuru huo uondolewe kwa sabbau wengi wa wafanyibiahsara hawa wanumia..hamna soko illhali ushuru katika bidhaa za mira ni ghali mno.’’ Kanario alisema.

Joho Hapo Jana aliweka wazi kuwa serikali yake haitatiza ushuru mizigo ya miraa inayoingia Mombasa  na kulingana nao tayari serikali ya Joho imeanza kutekeleza agizo hilo.

”Mizigo ambayo imefika Kongowea haijatozwa ushuru na maafisa wa kaunti ya Mombasa ishara tosha kuwa wameanza kutekeleza ahadi ya gavana Joho.” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *