709 300
Jamii ya Wanubi sasa wameendelea kushinikiza serikali kuwapa utambulisho kama moja ya makabila ya humu nchini.
Kulingana na afisa mkuu wa shirika la Nubians Right Forum Shaffi Ali wamefuata sheria kikamilifu kupitia bunge na tayari bunge hilo liliidhinisha hilo.
Sasa wametishia kufanya maandamano mpaka kule ikulu ikiwa hilo halitatimizwa na serikali kwa muda wa siku 30 zijazo.
‘‘Tumefuata sheria zote lazima tuskizwe kama rais hataskiza kwa siku hizo thelathini basi tutajikusanya tuandamane mpaka ikulu.” Shaffi alisema.
Aidha wanasema kuwa wanapitia magumu kupata vitambulisho na hilo si sawa kwani wanapigwa msasa mara kadhaa na hata kunyimwa haki hiyo wakati mwingine.