• Sat. Dec 3rd, 2022

Tambua Wanubi kama Kabila-Rais Kenyatta Ambiwa

Mar 22, 2022
124 300

Jamii ya  Wanubi sasa wameendelea kushinikiza serikali kuwapa utambulisho kama moja ya makabila ya humu nchini.

Kulingana na afisa mkuu wa shirika la Nubians Right Forum Shaffi Ali wamefuata sheria kikamilifu kupitia bunge na tayari bunge hilo liliidhinisha hilo.

Sasa wametishia kufanya maandamano mpaka kule ikulu ikiwa hilo halitatimizwa na serikali kwa muda wa siku 30 zijazo.

‘‘Tumefuata sheria zote lazima tuskizwe kama rais hataskiza kwa siku hizo thelathini basi tutajikusanya tuandamane mpaka ikulu.” Shaffi alisema.

Aidha wanasema kuwa wanapitia magumu kupata vitambulisho na hilo si sawa kwani wanapigwa msasa mara kadhaa na hata kunyimwa haki hiyo wakati mwingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *