Wale wanaoishi na ulemavu katika maeneo ya Pwani wameendelea kupata ugumu wa kupata kutambua haki zao na hata huduma za kisheria.
Hii ni kulingana na Wakili Shadrack Wambui wa shirika la Sheria Mtaani ambaye amekua Mombasa kwa ushirikiano na Baraza la Walemavu Nchini
Kulingana na Wambui taasisi husika bado haijawafikia jinsi invyotakikana kwa walemavu hao, ili kuwatambua na changamoto zinazonazowakumba .

Hii leo shirika hilo la Sheria Mtaani na maafisa kutoka baraza la walemavu nchini wametembea mitaa duni mbali mbali kaunti ya Mombasa ikiwemo Bombululu,Likoni katika nyumba wanakoishi walemavu ili kuwahamasisha kuhusu haki zao.
‘‘Tumeweza kuzungumza nao kuna usaidizi ambao tumepeana kama vile ushauri nasaha na hili si mwisho tutaendelea kushirikiana na baraza hili kuhakikisha kuwa tumefanya Zaidi…hii leo tumezuru sehemu mbali mbali ikiwemo Bombululu,Likoni ambapo tumezungumza na walemavu katika makaazi yao.’’ Wambui amesema.
Shughuli hiyo iling’oa nanga hapo juzi katika uwanja wa Tononoka na imetamatika leo.
