• Sat. May 3rd, 2025

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Maisha Bila Kafyu, Wananchi Washabikia Amri ya Rais

Oct 21, 2021
371 300

Wananchi wameendelea kufurahia kuondolewa kwa Kafyu. Wengi wameeleza jinsi biashara zao zitanoga na kuongezeka kwa Kuwa watafanya biashara kwa masaa ishirini na nne.


Wafanyabiashara katika kaunti ya Mombasa ni baadhi ya wale ambao wameonyesha kuridhika na hatua hii ya kufunguliwa kwa nchi.


“Ujumbe wa Rais hiyo Jana ulipenendeza mno. Namwombea maisha Marefu. Wananchi wamekuwa wanaishi maisha ya unyonge kutokea janga la Korona lilipoingia Kenya. Lakini sasa baada ya Kafyu kuondolewa, najua Sasa watu wengi watasafiri na kuja Mombasa kwa biashara nyingi,” alisema Dan Omweya.


Wanabiashara wengi walikuwa wakilalama kuathirika na masharti ya kutotembea usiku.


Aidha Omweya alisema ni matumaini Yao biashara zitanoga kwa Juma moja lijalo na uchumi Kuwa mzuri.
“Najua kazi tutaifanya kazi vizuri. Tutazingatia masharti ya kuosha mikono na kuvaa Barakoa,”aliongeza Omweya.


“Kupitia ujumbe wa Rais Jana tunashukuru Sana kwa Kuwa biashara ilikuwa imerudi chini Sana. Najua mwisho wa Juma hili au lijalo, tutakuwa tumerejelea hali ya kawaida katika biashara,”alisema Betty Leah.


Kwa miezi kumi na tisa kumekuwa sheria ya kutotoka nje usiku. Sehemu nyingine zikifungwa kwa wakati mmoja ilikuzuia kuenea maambukizi ya Virusi vya Korona.

Biashara nyingi zilirekodi kupoteza pesa nyingi huku nyingi zikifungwa na kupunguza idadi ya waajiri.

READ ALSO: Jaribio la Kujitoa Uhai Latibuka Baada ya Mshukiwa Kumuua Mkewe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *