619 300
Polisi katika eneo la Likoni wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayedai kuwa nabii na anafanya miujiza ya kuponya watu magonjwa na matatizo mengine.
Laban Mwangi wa kanisa la Jesus Winners Ministry Likoni anadaiwa kuwalaghai waumini wake maelfu ya pesa akidai kuwaponya matatizo yao yakiwemo utasa, kukosa kazi na magonjwa mengine.
Akithibitisha kukamatwa kwake mkuu wa polisi wa Likoni Joseph Karanja amesema kuwa haya yanajiri baada ya wanawake 7 kupiga ripoti kudai kulaghaiwa kwa ahadi kuwa wangeponywa kupitia miujiza.
Wanawake hao wakisema kuwa wanauza hadi vyombo vyao vya nyumbani kutafuta miujiza hiyo.Kwa sasa anazuiliwa na polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.