Maafisa wa Polisi katika Kaunti ya Kisumu wanamzuilia mwanafunzi wa Kidato Cha tatu aliyepatikana na furushi la bangi katika Shule ya Upili ya Rapogi eneo la Kombewo, Kaunti Ndogo ya Seme.
Walimu katika Shule hiyo waliwataarifu Maafisa hao kuwa Mvulana huyo amekuwa akiwapa wenzake mihadarati hiyo.
Chifu wa Kata ya Seme Magharibi, Nicholas Oguma amesema Kuwa hatua za haraka zilichukuliwa na Mvulana huyo alipatikana na misokoto kumi na moja ya Bangi.
Baada ya kufanya mahojiano na Mvulana huyo, alifichua alikopata bangi hiyo.
Chifu Oguna ambaye ndiye aliongoza Oparesheni hiyo, amedhibitisha Kuwa mwanamke aliyekuwa akimpa Mvulana huyo bangi alikamatwa na misokoto mia Saba na lita kumi na nne za Chang’aa.
Wawili hao walikamatwa na watafikishwa mahakamani ili kufunguliwa mashtaka.