Jambazi aliyekuwa amejihami kwa silaha alipigwa na Kuuawa na Wananchi huko Ruai.
Hii ni baada yake kuhusika kwa wizi wa kimabavu.
Kulingana na Ripoti ya Polisi Iliyoonekana na Taarifa News wanawake wawili waliokuwa wakielekea kazini mapema hiyo Jana, walivamiwa na majambazi watatu waliokuwa na bunduki katika eneo la Capital Hill Ruai.
“Wezi hao walikuwa katika shughuli zao za kawaida walikuwa wamepanga kuwavamia wawili hao, Anne Wanjiru na Lilian Mueni wakati waliposhambuliwa na Wananchi,” polisi walisema.
Afisa wa Polisi mwenye cheo Cha ‘Seargent’ Samuel Mutuku aliyekuwa njiani pia kuelekea kazini alishuhudia tukio hilo na kuwaamuru watatu hao kujisalimisha.
“Watatu hao walikataa kujisalimisha na badala yake wakaanza kumvamia askari yule. Lakini Mutuku mwenye tajriba katika kulinda mali na maisha ya Wananchi alipambana nao huku akimjeruhi mmoja wao wawili wakikwepa,” ilisoma Ripoti hiyo ya Polisi.
Mutuku aliwafuata wawili hao ambako walipanda Boda Boda iliyokuwa karibu lakini ikakataa kuwaka na wakakimbia kwa miguu.
Jambazi yule aliyekuwa amejeruhiwa alipigwa na Wananchi waliokuwa wajawa na ghadhabu huku wakimuuwa papo hapo.
Maafisa wa Polisi walikuwa wakiwarai Wananchi kutompiga jambazi huyo lakini Wananchi hawakuwaskiza.
Pikipiki ambayo iliwachwa na majambazi hao yenye usajili KMFL 494T ilichukuliwa na makachero wa DCI ilikuendeleza uchunguzi zaidi.
Simu waliokuwa wamempokonya mmoja wa Wanawake hao ilipatikana pia na Upangq Mrefu na ‘Machete.’