Mwakilishi wadi wa Mountain View Muarice Ochieng hatimaye ametoa msaada kwa wale waathiriwa wa moto katika mtaa duni wa Kangemi Gichagi.
Maurice akiwa katika ushirikiano na mbunge wa eneo hilo Tim Wanyonyi aliwapa waathiriwa hao chakula na hata godoro kwa kila mwathiriwa.
Kulingana na Maurice amefanya hivyo kujaribu kuwainua waathiriwa hao wa moto kurudi maisha yao tena.

‘‘Nataka kuwaambia pole kwa watathiriwa wa moto huu lakini pia leo hii nimewatembelea na ungaa,sukari,godoro na hata bidhaa zingine ili muanze tena kuishi na kurejea katika maisha yenu ya kawaida.’’Maurice alisema.
Aidhaa ametaka serikali ya kaunti kufanya hima na kuhakikisha kuwa kuna kituo cha moto kwa kila eneo bunge ili iwe rahisi kwao kukitokea moto.

‘‘Ni Jukumu la kaunti kuhakikisha kuwa kuna kituo kwa kila eneo bunge na hata wadi hiyo itasaidia kuzima moto wakati ufao… eneo hili kama kungekuwa na kituo karibuni basi athari haingekuwa kubwa jinsi tulivyoshuhudia.’’ Aliongeza.
Wanyonyi na Muarice wameapa kufanya kazi pamoja ili kunufaisha wakaazi wa eneo hilo.