Masomo yamerejelewa hii Leo katika eneo la Ol Moran kaunti ya Laikipia baada ya Shule kufungwa kwa muda.
Hii ni baada ya Shule kufungwa kwa kufuatia Mashambulizi ya Muda na Majambazi walokuwa wamejihami.
Eneo la Ol Moran lilitangzwa hatari kwa usalama baada ya Majambazi hao kuwacha wakaazi wengi bila makao huku Shule zaidi ya kumi zikiteketezwa.
Kwa Sasa, Serikali imeongeza Maafisa wa usalama wa kitengo Cha GSU katika eneo hilo wanaowalinda wanafunzi na Walimu katika mashule.
Juma lililopita, Waziri wa Usalama wa Ndani Daktari Fred Matiang’i alikita kambi katika eneo hilo ilikuhakikisha Kuwa Shule zinafunguliwa Leo.

Aidha Gavana Nderitu Mureithi alikuwa amewahakikishia wenyeji Kuwa shule zingefunguliwa kwa Kuwa Serikali iko mbioni kuhakikisha usalama upo dhabiti.
Awali, Mbunge wa Tiaty William Kamket na aliyekuwa Mbunge wa Laikipia Kaskazini William Lemourkel walifikishwa mahakamani na kustakiwa kwa Madai ya uchochezi Miongoni mwa wananchi.
Majambazi hao wanadaiwa kutumia silaha zenye nguvu Sana na ndio maana Maafisa wa GSU walipelekwa.