Wakaazi wa Kware sasa wanalia uharibifu wa mabomba ya sewage katika eneo hilo ambao unasababishwa na baadhi ya watu wanaoshirkiana na landlords.
Kulingana na mwakilishi wadi eneo hilo Rose Kula kundi hilo likiongozwa na jamaa kwa jina Karis ,wametoboa sewerlines na hivyyo maji ya kinyesi imekuwa ikitapakaa katika makaazi ya watu kule Kimondo kware.
Amesema wengi wanahangaika na ipo haja ya NMS kuja maramoja kuwachukulia hatua watu hawa.
‘‘Maji ya kinyesi kila mahali kwa sababu ya mtu anaitwa Karis amehitilafiana na kila kitu mazingira yamechafuka na maisha ya wakaazi wa Kimondo yako hatarini.’’ Kula alisema.
Kituo hiki pia kimememfikia jamaa huyo kwa jina Karis amabye amekuwa akihitilafiana na sewer lines sehemu hizo na kusababisha uchafuzi wa mazingira.
‘‘Ni kweli nimekuwa nikifanya hivyo lakini ni shida tuko nayo lakini hatujasaidiwa mimi nikaona ni toboea na niweke paipu ili sewage isitapakae pahali moja.’’ Alisema.
Tayari kituo hiki kimewasiliana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Nairobi City Water and Company Nahasion Muguna na amewahikikishia wakaazi hao kuwa hatua itachukuliwa mara moja, kurekebisha hilo na hata kuwakabili wanaovuruga na kuvunja paipu na mabomba hayo ya sewage mtaani humo.