• Tue. Apr 29th, 2025

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Familia yateketea Kwa Moto kajiado

Sep 3, 2021
618 300

Familia ya watu wa tano iliteketea usiku wa kuamkia Leo katika eneo la Mashuru Kaunti ya Kajiado.


Mama, wanawe watatu na mfanyikazi wao wa nyumbani ndio walioteketea wakati ambao mzee mwenye nyumba, Saitoti Maina hakuwepo.


Kulingana na Jonathan Sikongei, Naibu wa Chifu katika eneo hilo, moto huo uliotokea mida ya saa nne ulisababoshwa na hitilafu za umeme.

“Tulipata habari Kuwa watu watano wameangamia kwenye moto wa stima tukakimbia hapa kujaribu kuwaokoa lakini haikuwezekana,”alisema Sikongei.


Mwandani wa familia hiyo, Paul Maina alisema kuwa mtungi wa gesi ulipatikana hapo baada ya moto kuzimwa.


“Moto ulianza saa nne usiku kutokana na hitilafu za umeme,”Maina aliambia Taarifa News.


Miili ya watano hao imepelekwa Makafani ya hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kajiado huku uchunguzi zaidi ukiendelezwa kubani chanzo Cha moto huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *