Kamati ya Uhasibu bunge la kaunti ya Nairobi sasa limemteua mwakilishi wodi wa Mabatini Wilfred Oluoch Odalo kama mwenyekiti wa kamati hiyo na sasa atahudumu kwa mwaka mmoja uliosalia.
Chama cha ODM kiliondoa wanakamati wake PAC lakini sasa oparesheni za kamati hiyo zimerejea baada bunge kupitisha majina ya wanakamati Alhamisi iliopita.
‘‘Ninataka kushukuru chama changu cha ODM,kinara wetu Raila Odinga,viongozi wa bunge na hata wanakamati kwa kuwa na imani kwangu..kamati hii ilivunjwa kwa sababu ya tofauti ya hapa na pale sisi tukaondolewa na chama lakini tumerejea na tuko tayari kupeana huduma kikamilifu.’’ Odalo alisema.
Kulingana na Oluoch yuko tayari kuhakikisha kuwa mali ya umma imelindwa kwani kupitia uongozi wake hapo awali kama kamati wameweza kurejesha shamba la kaunti ambapo hoteli ya Ball and Green Kule Parklands ili jengwa, mbali na hayo wameweza kushirikiana na tumeya kupambana na EACC katika uchunguzi wao na kuhakikisha kuwa mbunge wa Mathira Rigathi Gachagwa ameandamwa hii ni baada ya kuhusika katika unyakuzi wa shamba la umma kule Mombasa road.
‘‘Kama mwenyekiti kuna mengi ya kujivunia tumejaribu kila tuwezalo kulinda mali ya umma wa hivi ni mbunge Rigathi Gachagwa ambaye alihusika katika unyakuzi wa shamba la umma Mombasa road tumeshirikiana na EACC na kwa sasa ameandamwa na tume hiyo.. tumefanya mengi nab ado tutaendelea.’’ Rigathi alisema