• Wed. Sep 18th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Watu Wawili wanaswa kwa Wizi wa Umeme

May 17, 2021
820 300

 Maafisa wa polisi wanawazuilia wanaume wawili waliokuwa miongoni mwa watu nane wanaodaiwa kujifanya kuwa wafanyikazi wa Kampuni ya umeme ya Kenya Power.

Polisi kule Kingeru, chini ya kituo cha polisi cha Kabete Kaunti ya Kiambu wanawazuilia wanaume baada ya madai kuibuka kuwa wamekuwa wakiiba nyaya za umeme na pia taa zinapoekwa na serikali ya kaunti ya Kiambu. Wakati huo. huo Malori mawili yamenswa yakisafirisha baadhi ya bidhaa zinazoshukiwa kuibwa.

“Tumepata vijana wawili wa hapa, Kuna mmoja anaitwa karwea na mwingine anaitwa koge. Wakaniambia Wanja kuna hawa watu wame park Lorry hapa wanatoa mataa na hatuwaelewi. Nikawasimamisha nikawauliza mbona mnabeba taa zetu na vikingi wakasema wametumwa na kaunti government. Nikawambia Serikali ya kaunti nafanya nawao mbona mimi sijui wakasema tena wametumwa na Kampuni ya Umeme. Kuuliza mbunge wetu ambaye ndiye ameweka taa hizi, akasema hajui. Nikapigia OCPD simu akatuma polisi. Tumewafuata sita wametoroka tumewakamata wawili,” aliripoti Wanja.

Inadaiwa wanaume hawa waligunduliwa kuwa na njama baada ya wenyeji wa eneo hilo kuibua maswali kuwahusu.

Wakijitetea wawili hao wamesema kuwa, walitumwa na maafisa wa Limuru wa Umeme na walitaka waulizwe ili kudhibitisha. Aidha wameongeza kuwa walichokuwa wanakifanya si kinyume cha sheria kwa kuwa ilikuwa inasabaisha hitilafu za umeme

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *