• Thu. Sep 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Watu waliomvamia na Kumpora MCA kufikishwa mahakamani

Jun 23, 2021
412 300

Zaidi ya watu wanne watafikishwa mahakamani hapo kesho baada baada ya kumvamia na kuharibu gari la Mwakilishi wodi wa Makongeni Peter Imwatok.

Mwakilishi Wodi huyo alikuwa amehudhuria Mashindano ya Soka siku ya jumamosi katika eneo hilo na hapo ndipo alipovamiwa.

Akizungumza na Taarifa, Mheshimiwa Imwatok alisema kuwa alikuwa amehududhuria mashindano ya soka yaliyo andaliwa na Ofisi yake kwa ushirikiano na KARA na alishtuka kuwaona vijana wakimvamia na kumwibia hela, huku wakiharibu gari lake na kuwajeruhi walinzi wake.

“Mimi kama mwakilishi wodi wa Makongeni sitaruhusu mambo kama haya kutokea Makongeni. Vijana hawa walituvamia tukiwa tunatizama mashindano ya soka na waliwajeruhi walinzi Wangu na kuharibu gari langu pia. Wale wanaoleta fujo hizi ni heri wasihudhurie mikutano yangu,” alisema Imwatok.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *