• Wed. Sep 18th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Watu 10 mashakani baada ya Kunywa pombe yenye sumu

Jul 12, 2021
347 300

Mtu mmoja amefariki huku tisa wakilazwa hospitalini katika mji wa Nyahururu baada ya kubugia Pombe haramu.

Kulingana na Daktari Felix Masongo ambaye ndiye anawashughulikia katika hospiutali ya Rufaa ya Kaunti ya Nyahururu, wagonjwa hao walianza kuugua Jumapili asubuhi. Amesema kuwa walikuwa wakiumwa na tumbo, wakiendesha na kutapika walipofikishwa hospitalini.

Daktari huyo ameongeza kuwa wagonjwa hao walichukuliwa katika vitongoji tofauti lakini wengi walichukuliwa karibia sehemu moja. Watatu t6ayari washatibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku wengine bado wakaendelea kupokea matibabu.

Aidha Daktari ameongeza kuwa bado hawajatambua kinywaji haswa walichotumia lakini wamebaini kuwa kilikuwa na chembechembe za sumu.

Kulingana na wenyeji wa eneo hilio, walioathirika walikuwa wamehudhuria sherehe ambako mwenye baa aliwaalika baada ya Mkewe kujifungua. Pia wameiomba serikali kufunga maeneo yote ya burudani ambayo hayana Leseni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *