• Fri. Apr 19th, 2024

Watoto Wanaoishi na Ulemavu Wakumbukwa na Wafadhili Kibra

Jul 29, 2021
390 300

Wakaazi eneo la Kibera wamebahatika hii Leo kupewa Viti vya Magurudumu kwa wanawao wenye Ulemavu kutoka kwa mfadhili, Michael Panther ambaye ndiye mwanzilishi wa Shirika la Living with Hope Africa.


Michael ambaye pia ni mlemavu, amekuwa akiwasaidia wakenya wenye Ulemavu kote nchini. Leo hii akishirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la World Leaders of Tomorrow (WLT) wamewapatia watoto themanini viti hivyo vya Magurudumu.


Akizungumza na Taarifa News wakati wa kutoa misaada hiyo, Bwana Michael amewahimiza wananchi kutowaficha walemavu kwa kuwa ni watu wa Kawaida na wakifichwa watapitwa na misaada kama hiyo. Aidha amehimiza serikali na Kampuni mbali mbali kuwaajiri walemavu bila ya kuwabagua.


“Wazazi wasiwafiche watoto walemavu. Hilo linafanya watoto wengi kupitwa na misaada. Najua katika jamii nyingi Afrika watoto hao wanachukuliwa kama misimu isiyo takikana na Hilo ni kosa Sana. Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali na Makampuni pia ziwaajiri walemavu. Aidha serikali pia yaweza kuungana na Mashirika yasiyo ya Serikali katika kuwafadhili na Kuwainua walemavu,” alisema Michael.


Watoto hao walemavu na wazazi ambao Wana wao walipewa viti hivyo hawakuficha furaha yao.


Walifurahi Sana kwa msaada huo na kuwaambia wenzao walio na watoto walemavu kujitokeza kwani mtoto ni Mtoto hata awe mlemavu.


” Huwa inahuzunisha kuwaona watoto wetu wakibaguliwa. Hata ukitoka kwa ajili ya shughuli zao za kutafuta, wanashindwa yule atakaye baki na wanao. Sasa hata nikienda kanisa tutaenda pamoja,”alisema Caroline Achieng.


” Majirani wengine hata wanakosa kujihisisha na sisi ambao tuna watoto walemavu, kisa eti tunaweza kuwasababishia mikosi. Watu wasiwafiche watoto walemavu. Nafurahi kwa kuwa tangia Mwanangu azaliwe Sasa ana miaka kumi na moja hajawahi kutumia kiti hiki. Pia huwa ni vigumu kwake kukalia kiti Cha Kawaida,” aliongeza Rosemary.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *