• Thu. Apr 18th, 2024

Watoto 3 Wateketea Ndani ya Nyumba Elburgon

Sep 29, 2021
316 300

Watoto wa tatu wenye umri wa miaka minne, Tano na sita waliangamia jana baada ya moto kuteketeza nyumba yao katika eneo la Turi, Elburgon kaunti ya Nakuru.


Kulingana na baba ya watoto hao, Bwana George Omoso ambaye amekuwa akiwalea peke yake, alikuwa ametoka nje kununua Chajio moto huo ulipozuka.


Bwana George alieleza Taarifa News kuwa aliporejea kutoka kwenye duka alipata tu majivu ya nyumba kila kitu kikiwa kimeshachomeka na wanawe waliokuwa ndani ya nyumba.


Chanzo cha moto bado hakijajulikana kwa kuwa watoto hao walikuwa peke yao wakati wa Tukio hilo.


“Ni moto ilichoma nyumba, nilikuwa tao nikaskia kuna moto nikafika nipo nilipata wamechomekea kwa chumba,” Alisema George.


Baba huyu amekuwa akiishi na wanawe tangia mwaka elfu mbili Kumi na Nane wakipoikosana na mkewe na akamwacha na watoto hao ambao amekuwa akiwalea pekeake.


OCPD wa kaunti ya Molo Mwenda Muthama amethibitisha tukio hilo akisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha moto.

READ ALSO:MCA wa Mountain View Afanya Ugavi Wa Msaada Kwa Waathiriwa wa Moto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *