• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wapangaji Makongeni Wakabana na Polisi Kuhusu Nyumba za Idara ya Reli

May 20, 2021
539 300


Maafisa wa Polisi Asubuhi ya Leo wamewatawanya wakaazi wa Makongeni baada ya Maafisa wa Mpango wa Kenya Railways Retirement Benefit Scheme kuvamia makazi yao ili kuanzisha Kampuni mpya ya usalama.

Wakaazi wa Makongeni walipogundua mpango huo waliandaa maandamano ambayo yamepelekea polisi kutumia vitoa machozi ili kuwatawanya.

“Hatutakubali Mtu yeyote atufukuze bila kufuata sheria. Mnamo tarehe 17 korti ilitoa amri ya kuzuilia kufukuzwa, lakini mpango huo na polisi wamekataa kutii maagizo ya Korti,” Walilalama Wapangaji.

Kulingana na Mwakilishi Wodi wa Makongeni, Mheshimiwa Peter Imwatok, walipata agizo kutoka Kortini ambalo linazuilia kufukuzwa kwa wapangaji hadi kesi itakapo sikizwa tarehe 31Mei.

“Nimeshtuka wanataka kuwaondoa watu wetu na bado agizo la korti lipo na wamehudumiwa kwa wakati . wacha Mkurugenzi Mtendaji mpya katika mpango huo atii sheria kwa sababu kama ilivyo wapangaji hawaendi popote mpaka mahakama iamue suala hili.” Imwatok alisema.

Kulingana na amri ya Korti ambayo Taarifa news waliiona, inasema kuwa: “Maombi ya tarehe 17 Mei 2021 yalizingatiwa kama maombi ya dharura 2 yaliyotolewa kwa muda mfupi basi ombi litolewe kwa usikilizaji wa pande mbili mbele ya mheshimiwa Muholi mnamo 31 Mei 2021.”

Katika ombi lililowasilishwa katika mahakama ya Milimani, wapangaji 4,800 wanataka KRSRBS Kungoja ombi lao kusikizwa na kuamuliwa. Pia wanataka waweze kupewa huduma za mifumo ya maji taka, usambazaji wa maji na vifaa vya choo, uzio wa mzunguko, ukusanyaji wa takataka na huduma zingine za kijamii zinazotumiwa na wakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *