Na Taarifa Team
Mbunge wa Kibra Imran Okoth sasa amewasilisha petition kutoka kundi la Nubians Right Forum kuhusu malalamishi ya unyanyasaji amabyo jamii hiyo inapitia nchini.
Imran tayari amekabidhi bunge la kitaifa Malamishi hayo na spika Muturi ameiwasilisha kwa kamati ya usalama bungeni.
Kulingana na mwenyekiti wa Nubians Right Forum Shafi Ali wanataka maswala ya usajili na haki zao kuheshimiwa.
‘‘Tunasubiri tu kuitwa na kamati hii ili tukae meza moja na wahusika wote kwani ikiwa hali itaendelea kuwa hivi basi mnubi hatakuwa na haki tena nchini,hatuna vitambulisho,hatuna kazi tunabaguliwa na hakuna anayetuskiza haya lazima yarekebishwe,’’ Shaffie alieleza.
Pia wameomba bunge kuchukulia hilo na uzito kwani hawapati nafasi za kazi,wanubi wengi pia hawana vitambulisho.
Kamati hiyo sasa itaskiza malalamishi ya jamii hiyo baadae iwaalike wizara ya usalama wa ndani pia kupata upande wao kabla ya kuandika mapendekezo yake.