• Wed. Jun 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wanafunzi Watakiwa Kufungua Shule Licha ya Uhaba wa Karo

May 10, 2021
673 300

By Antonyt Ford

Shule zinapofunguliwa hii Leo, Wazazi wengi wamewaomba Walimu kutowafukuza wanao kutokana na madeni ya Karo.

Wazazi wanasema kuwa janga la virusi vya korona vimewafanya kukosa hela lakini wanajitahidi kuhakikisha wamewalipia wanao.

“Walimu wakuu wasiwafukuze watoto, tunajitahidi ili kuhakikisha tumelipa karo za muhula huu. Maisha sasa ni magumu kwa sababu tumepoteza kazi na lazima tufanye vibarua ili kukidhi mahitaji ya familia zet,’’ Ann Nderitu mzazi alisema.

Awali, waziri wa elimu Professa George Magoha alikuwa ametowa onyo kwa Waalimu wakuu ambao watapatikana wakiwatuma wanafunzi nyumbani kwa sababu ya karo.

Akizungumza hii Leo, mwakilishi wodi mteule katika kaunti ya Nairobi ambaye pia ni mtaalam wa maswala ya elimu Mary Arivitza Mwami, amesema kuwa serikali ya Kaunti ya Nairobi imeshatoa takribani shilingi Bilioni tatu nukta nne kwa kila wodi ili kuwalipia wanafunzi karo.

Aidha Mheshimiwa Arivitza amewaomba Wazazi kuwaacha wanao waende shuleni kwa sababu serikali huwa inawalipia kiwango cha asilimia hamsini ya karo na hivyo basi si ghali sana.

Mary pia amewahimiza wanafunzi kutia fora masomoni ili kuwa watu wa maana katika maisha yao ya baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *