• Thu. Mar 28th, 2024

Wanafunzi Warai Serikali Kuwapa Mkopo wa Helb

May 25, 2021
314 300

Wanafunzi wa vyuo vikuu sasa wanataka serikali kutafuta njia mbadala ya kufadhili mkopo wanaopata kutoka bodi ya HELB wakisema kuwa ikiwa pesa hizo zitakosa kama inavyosemwa na bodi hiyo basi masomo ya wananfunzi wengi yaatathirika.

Wanafunzi chuo kikuu cha Nairobi wakiongozwa na Maxwel Magawi wanasema hawaamini pesa za mkopo za wanafunzi zinawezakosekana licha ya pesa za BBI kukwepo wakitaka serikali kuwapa fedha za HELB.

“Wanajihisi vipi ikiwa wanapesa ya kuendesha BBI na mikopo ya wanafunzi hakuna wanataka tufanye vipi na hii pesa ndio kila kitu kwa maisha yetu chuoni.” Alisema.

Wamesema kuwa wengi wanafunzi wanaotoka familia maskini wanategemea HELB kugharamia karo zao na hivyo basi si ya kujivinjari.

Hivi majuzi bodi ya HELB kupitia afisa mkuu mtendaji wake Charles Ringera aliweka wake wazi kwamba hawana fedha za mkopo kwa wanafunzi 95,000 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *