• Thu. Jun 20th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Waliojaribu Kumfurusha Imwatok kama Kiranja Wakabwa na ODM

May 25, 2021
416 300


Katibu mkuu wa chama cha ODM sasa anasema kuwa chama hicho kitaadhibu wakilishi wote waliojaribu kufanyia mabadiliko afisi ya kiranja mkuu bila kujali mwelekeo uliotolewa na chama, ukikataza hilo.
Kulingana na Sifuna hapo kesho wakilishi hao saba waliojaribu kumtoa afisni kiranja Peter Imwatok watapokea barua.

Kulingana na Sifuna kesho wanafanya mkutano na wakuu wa chama hicho na kuwapa barua za kinidhamu wakilishi hao kwani hawatakubali wanachama wakose kufuata sera za ODM.

Sifuna ameweka wazi kuwa aliandika barua ya kusimamisha kuondolewa kwa Imwatok lakini wengine walipuuza.

READ ALSO: MCAs who took part in ‘illegal’ ouster to be punished tomorrow


‘‘Kesho tunakutana tutaangazia swala hilo na mabunge mengine na wajumbe ha watakuwa wamepata barua,hatutaruhusu sarakasi kama hiyo kuendeleza na MCA wetu,’’ Sifuna alisema.

Mbali na hayo naibu spika Geoffrey Majiwa ametaka bunge hilo kuchunguza jinsi stakabadhi zilizotumika katika kikao cha kujaribu kumtoa mamlakani Imwatok zilivyopatikana kwani yeye hakujua lolote.

‘‘Nataka kujua walipata idhinisho kutoka kwa ofisi yangu kivipi na mimi sikuidhinisha chochote, Kamangu si naibu spika ni mwenyekiti wa wenyekiti ni vipi alitumia stamp yangu katika kikao cha kumng’atua Imwatok,’’ Majiwa alisema kwenye barua kwa spika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *