Walinzi Watatu wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Kivaywa Kaunti ya Kakamega wamefariki huku wawili wakinusurika na majeraha baada ya kuvamiwa na majambazi usiku wa kuamkia hii Leo.
Edward Malala 40,Henry Khaoya 55 na Evans Wanyonyi waliuawa huku Situma Situko na Lucy Wanja wakinusurika na majeraha.
Miili ya Waliofariki imepelekwa katika Makafani ya Webuye huku Wawili walioponyoka kifo wakitibiwa katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Webuye.
Majambazi hao walifanikiwa kutoroka na Runinga, kipatakilishi na Pesa Shilingi Elfu mia Moja Hamsini.
Akizungumza na Taarifa News, OCPD wa eneo la Matete Thomas Ototo amesema uchunguzi umeanzishwa ili kuwapata walio tekeleza uovu huo.
“Maafisa wetu wamefika shuleni humo ma wanaendeleza uchunguzi,”alisema Bwana Ototo.