Wakilishi wadi Nairobi sasa wanataka serikali ya kaunti ya Nairobi kuwapa cheki ili waandikie wanafunzi wanaopata basari lakini si vocha kwani bila cheki waalimu wengine wakuu wanapokea vocha hizo na kudinda tena kuwa hawajapokea pesa.
Maurice Ochieng mwakilishi wodi Mountain View anasema kuwa huo ndio njia pekee ya kuzima walimu hao wakuu wafisadi na kuleta uwajibikaji miongoni mwao.
‘‘Tume kuwa na shida kubwa na hawa wakuu wa shule kwa sababu tunapeana vocha ya karo kwa wanafunzi lakini baadae unaskia kwamba hawakupokea pesa…kumaliza kabisa changamoto hii tupewe cheki tuandikie hawa wanafunzi itasadia pakubwa kumaliza udanganyifu huu,’’ mwakilishi huyo alisema.
Ametaka serikali ya kaunti kutekekeleza hoja iliopitishwa na bunge la kaunti Nairobi ya kutumia cheki Kwani hilo kama halitafanyika basi serikali itaendelea kupoteza pesa.
‘‘Uwajibikaji ni kitu ya maana tayari tumepitisha hoja ya kuhakikisha kuwa tunatumia cheki na kwa serikali ya kaunti mtekeleze hoja hiyo ili mwaka huu wa kifedha tuanze mara moja kupeana cheki laki sio vocha tena.’’ Maurice aliongeza.
Kila mwakilishi wadi hupokea shilingi milioni 3.5 za basari lakini wakaongezwa shilingi milioni moja na sasa watapokea shilingi milioni 4.5. mwaka huu wa kifedha.