• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wakaazi waandamana baada ya kupotea kwa Mwenda Mbijiwe

Jul 8, 2021
302 300

Wakaazi Katika eneo la Sirmon-Timau waliandamana wakitaka uchunguzi ufanywe kwa haraka ili kubaini aliko kijana wa umri wa Makamu aliyepotea takribani mwezi mmoja Sasa.

Mwenda Mbijiwe aliripotiwa kutoweka mnamo Juni 12 mwaka huu alipokuwa akisafiri kurejea Timau akitoka Nairobi.

Simu yake na gari alilokuwa alitumia kusafiri hazijulikani zilipo kwa kuwa simu yake imezimwa tangia wakati huo.

Aidha, babake aliripoti kupokea simu ya mtu asiyemjua akiuliza iwapo Mwenda aliwasili siku hiyo alipokuwa akisafiri. Pia wazazi wake wameomba Maafisa wa Polisi kuwasaidia ijulikane ni wapi alipo hata kama ameaga waweze kuuzika mwili.

“Tunaomba kujua Kijana wetu yuko wapi. Hata kama aliuawa basi tuonyeshwe mwili wake ulipo ili tuuzike.
Katika madai ya wananchi hao, wanasema kuwa huenda Mwenda aliuawa na wanasiasa Wenza ambao amekuwa akibishana nao tokea kufeli katika uchaguzi uliopita.

Naibu Kamshina was Meru ambako waliandamana hadi kwa Afisi zake, amewaomba kuwa watulivu na uchunguzi utakapokamilika atawapa jibu kupitia Mwakilishi wodi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *