• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Wahudumu wa matatu wakataa malipo ya nauli kupitia simu

Jun 14, 2021
347 300

Huenda huduma za kulipa nauli kwa njia ya simu zikatupiliwa mbali baada ya abiria wengi kutuhumiwa kuregesha pesa ambazo huwa wametuma.

Tukizungumza na mhudumu mmoja wa matatu moja iliyokuwa ikitoka Kitengela kuja mjini,amesema kuwa ana wasiwasi wa kutumiwa nauli kwa simu kwa kuwa wateja wengi huregesha pesa baada ya kutuma.

“unaweza ona abiria amevalia vizuri ukafikiri eti hawezi kuregesha pesa kumbe tabia ni ile ile. Siku moja nimeona mzee mwingine mwenye umri wa juu lakini baada yake kulipa shilingi mia nne alijiregeshea punde aliposhuka kwenye matatu,” alisema mhudumu huyo.

Tulipotaka kufahamu iwapo wao huripoti visa hivi katika vituo vya polisi walisema kuwa huwa ni kazi bure kwa kuwa maafisa wa askari huwaitisha hongo kabla yao kusaidiwa na hata mara nyingi hawapati usaidizi.

“Ukienda kwa Polisi labda kesi ni ya nauli ya shilingi hamsini na wanakuitisha shilingi mia moja. Sasa inakuwa unawapa pesa za bure,” alisema dereva mmoja.

Sasa wito unatolewa kwa Safaricom, Airtel na wengineo ili waweze kukomesha visa hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *