Wahudumu wa afya Nairobi chini ya usimamaiza wa NMS wametishia kushiriki maandmano ikiwa hawatapokea mishara yao ya mwezi Julai siku mbili zijazo.
Katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini KNUN tawi la Nairobi Boaz Onchari anasema kuwa wahudumu wa afya hawajapokea mishahara yao ya mwezi Julai na viongozi wa kitengo cha NMS wamewapa mgongo na mpaka sasa hawajui ni lini wanapokea pesa zao.
‘‘Tulifanya makubaliano nao kuwa kufikia tarehe tano wawe wanalipa mishahara lakini kwa sasa hatujui ni vipi hili limekiukwa na tumesalia tukihangaika huku mabosi hao wa NMS wakiendelea kutupuuza…tuna watoto tunahitaji kulipa kodi za nyumba wanataka tufanye vipi,’’ Boaz aliambia wanahabari
Pia wameshtumu utendakazi wa NMS wakitaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati la sivyo wako tayari kurejea katika uongozi wa serikali ya kaunti.
‘‘NMS iliapa kulinda haki zetu kwa sasa ni mwezi kumi na sita na hakuna cha mno cha kuzungumzia tukiangalia maisha ya wafanyikazi ni shida tupu na tuko tayari kurudi kwa serikali ya kaunti..hata mama anaweza.’’ Onchari aliongeza.
Brown Ashira wa chama cha wahudumu wa afya khps kwa upande wake amesema kuwa ikiwa siku hizo mbili zitakamilika bila kupata mishahara basi wataingia barabarani kushinikiza NMS kulipa fedha hizo
‘‘Hatutakaa chini na kuwatazama tukiwa njaa,baada ya siku mbili tutajitokeza wahudumu wote na tuingie kwenye maandamano.’’ Alisema.