• Thu. Mar 28th, 2024

Wafanyi Kazi wa afya Wagoma kulalamikia mshahara

Jun 22, 2021
239 300

Wafanyikazi katika hospitali ya Kaunti ya Kajiado wameandamana kulalamikia kucheleweshwa kwa mishahara yao kwa miezi tano.


Wafanyikazi hao ambao hufanya Kazi kama vibarua wanasema kuwa familia zao zinapitia hali ngumu Sana na kwa sasa hawajaweza kuwalipia wanao Karo, kununua Chakula na mahitaji Mengine.


“Sisi tunafanya Kazi hapa kwa uchafu Sana. Kubeba placenta za mama ambao wamezaa, kuosha matapishi ya Watu. Hatuna hata vifaa vya kujilinda…”alisema mfanyikazi mmoja.


“Sisi kama walinzi, huwa tunafika kazini mapema Sana, lakini kwa hata Kaunti ya Kajiado haioni hayo,”aliongeza Mlinzi wa hospitali.


Aidha wanasema kuwa wakijaribu kuulizia Mishahara yao, wanatishiwa kuwakutaletwa wafanyikazi wengine wapya.


“Tukijaribu hata kuulizia mbona hatujalipwa, tunaambiwa wataletwa watu wengine nasi tufutwe. Tunataka hata iwapo watu wengine wataletwa wapewe Mishahara kwa wakati unaofaa,” alisema mfanyikazi mwingine.


Mwishoni mwa mwaka jana wafanyikazi hao waliandamana pia kulalamikia ucheleweshaji wa mishahara bado na wakaahidiwa kusuluhishiwa swala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *