288 300
Kamati ya Fedha katika Bunge la Taifa limepinga kuongezwa kwa ushuru kwa bidhaa za Maziwa na Bodaboda.
Kulingana na Bajeti ya mwaka 2021/2022 , Waziri wa Fedha alikuwa amependekeza kuongezwa kwa ushuru wa maziwa na Bodaboda.
Akizungumza katika kikao Cha Kamati hiyo, Mwakilishi wa akina Mama Kaunti ya Homa Bay, Gladys Wanga amesema kuwa sio sawa bidhaa kama hizi kuongezwa ushuru kwa kuwa zinategemewa na Wananchi wa Kawaida.
” Ni vibaya kuongeza ushuru kwa bidhaa kama mkate wa Kawaida. Hiki ni chakula kinachotumiwa Sana na familia za Kawaida nchini,”alisema Wanga.
Aidha ameongeza kuwa ni Sawa kwa ushuru wa Kampuni za Kamari kuongezwa hadi asilimia 30%.