Baadhi ya viongozi wa kisiasa kule Embakasi South Nairobi sasa wanataka kinara wa ODM Raila Amollo Odinga kuendelea kushirikiana na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka katika siasa za kitaifa mwaka wa elfu 2022.
Mwakilishi wadi wa Kware Rose Kula anasema viongozi hao wawili wana mtazamo mzuri kwa taifa na ipo haja ya wao kufanya kazi pamoja tena.
‘‘Naomba kama mwanamke na kwa unyenyekevu wa nchi hii, kaa na baba yangu Raila Amollo Odinga mtupe mwelekeo…Mimi kama Rose nikiona uko kando na Raila yuko Kando basi Nina mshutuko ..kwa sababu hii wakenya wa kawaida wako wengi kuliko wale wanalia.” Rose alisema.
‘‘Ukienda ukae chini nione umetupatia mwelekeo hata hapa chini mashinani Mwananchi wa kawaida atakua na mwelekeo.”aliongeza
Walikuwa wanazungumza katika kanisa moja kule Embakasi South hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali sehemu hiyo.