Vijana katika Wodi ya Viwandani Kaunti Ndogo ya Makadara wamepewa nafasi ya kujiunga na shule ya Uendeshaji wa Magari kupitia Mradi wa kuwaweza na Kuwainua vijana kupitia Mwakilishi wodi wao, Mheshimiwa David Mbithi na Mbunge George Aladwa.
Vijana hao takribani mia tatu hivi wataweza kujiunga na Shule ya Uendeshaji Magari ya Rocky Kutokana na ufadhili wa shilingi Elfu mia Tano kutoka kwake Aladwa.
Pia akina Mama watapata shilingi Elfu mia Tano katika Mradi huo wa kuinuliwa na kupigwa jeki.
Akizungumza katika Afisi za Wodi ya Viwandani, Msaidizi wa David Mbithi alimshukuru Aladwa kwa kuungana na Mbithi katika Kuwainua vijana hao.
” Nashukuru waheshimiwa Aladwa na Mbithi kwa mradi huu. Sisi tunafanya mambo yetu kwa uwazi na hatuna ubaguzi. Wale ambao wanachukuliwa wasipo fika shuleni, simu hupigwa kutoka Ofisi za Rocky na mwanafunzi mwingine anachuwa nafasi ya yule asiyehudhuriwa huchukuliwa na mwingine,”alisema Frank.
Kiongozi wa Vijana wodi ya Viwandi, Jilly alimshukuru Mheshimiwa David Mbithi kwa mradi huo kwa kuwa watapata ujuzi utakao wasaidia.
” Nashukuru Mwakilishi wodi wetu kwa mradi huu. Uendeshaji Magari ni kazi nzuri na vijana watapata ujuzi utakao wasaidia, haswa kwa kuwa wanapelekwa katika shule iliyoidhinishwa na watapewa vyeti halali na hawatasumbuliwa kamwe,”alisema Jill.
Wanafunzi hao pia waliwashukuru viongozi hao, huku wale wa kike wakiwahimiza wenzao kujitokeza na kuwacha ubaguzi kuwa kuendesha Magari ni kazi ya wanaume pekee.
” Natarajia cheti halali Cha kisasa. Yale mambo ya vichochoro yashapitwa na wakati. Sasa tutakuwa na ujuzi utakao tusaidia kupata kazi. Nawahimiza akina Dada wajitokeze kwa kuwa hii ni kazi yetu sote, walisema kwa pamoja.