820 300
Kamishna wa eneo la Nyanza Magu Mutindika amepiga marufuku utumizi wa Magari ya shule na kanisa katika shughuli za Mazishi na harusi katika eneo hilo.
Kulingana na kamishna huyo hii ni mojawapo ya njia za kupunguza kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.
“Kutokana na kupanda kwa idadi ya wanapoambukizwa virusi vya Korona, mabasi ya shule, vyuo na kanisa zisitumike katika kuwasafirisha watu kwenye harusi au matanga,” alisema Magu
Maafisa wa Polisi wameelekezwa kuhakikisha hakuna gari lolote la shule linatumika kama ilivyoagizwa.
“Mtahakikisha masharti haya yanafuatwa mpaka maagizo mengine yatakapotolewa,”aliongeza Magu.