Polisi kaskazini mwa Uganda, katika Wilaya ya Moroto wameanza kuwakamata watu wanaonunua chapati tano au zaidi, wakishuku huenda wanawalisha wezi wa mifugo katika eneo hilo, Kama ilivyoripoti radio moja nchini humo.
“Tumepokea taarifa kwamba wale wanaonunua chapati nyingi wanawapelekea wapiganaji misituni,” Micheal Longole, msemaji wa polisi wa Karamoja, alinukuliwa.
Alisema kukomesha usafirishaji wa chakula kwa wezi hao huenda kukawalazimu kutoka mafichoni na kuwasilisha silaha zao.
Mwanaharakati wa amani wa eneo hilo Mark Koryang alisema mpango huo hautafaulu “Hawa wapiganaji wanaweza kuishi bila hata kula chapati,” alisema. Mkazi mwingine.
Aidha maafisa wa usalama wanahitaji kufanya kazi na watu wa eneo hilo ili kukabiliana na ukosefu wa usalama katika jimbo hilo.
Edrine Mawanda, Msemaji wa kitengo cha jeshi anayefanya zoezi hilo, aliiambia radio hiyo Kuwa bunduki 58 zimepatikana katika eneo hilo tangu zoezi la upokonyaji silaha lilipoanza mnamo Julai 17.