• Fri. May 24th, 2024

Uhuru Aonyesha Kutoridhishwa na hatua ya mahakama

Jun 1, 2021
247 300

Akihutibia taifa katika sherehe za kuadhimisha Madaraka za 58 katika kaunti ya Kisumu, Rais Kenyatta amesema kuwa japo mahakama ni huru na haifai kuingiliwa katika utenda kazi wake, ni vyema itilie maanani hitaji la wengi.

Rais ameonyesha wazi kutoridhishwa na hatua ya mahakama ya kusitisha mageuzi ya Katiba kupitia mchakato wa BBI.

Ameongeza kuwa kila mtu hata wale wanaopinga mchakato huo wa BBI wanajua inamanufaa mengi kwa wananchi lakini wanapinga kwa sababu zao wenyewe na hawafikirii manufaa yake kwa wananchi.

“Wanapinga BBI sio kwa sababu ya Yale ambayo yamo ndani yake bali kwa sababu zao wenyewe. Hawafikirii kama wanzilishi wataifa letu ambao walifikiria kwa manufaa ya kila mmoja,”alisema Rais Kenyatta.

Halikadhalika, Rais Kenyatta ametetea mwafaka baina yake na Kiongozi wa ODM Raila Odinga akisema kuwa, salamu baina yao maarufu kama ‘handshake’ limefanya pawe na Amani nchini.

“Nataka kumpongeza Ndugu yangu Raila kwa kutojali Masilahi yake binafsi bali ya Amani ya wananchi,”aliongeza Rais Kenyatta.

Aidha Rais ametumia fursa hiyo kulezea mafanikio ya serikali tokea kuchukua hatamu za uongozi. Amelinganisha mafanikio yake na serikali tatu zilizomtangilia na nyakati za ukoloni.

Miradi wa Ujenzi ya Barabara, kukarabatiwa kwa Reli ya Zamani na kupeana kwa hati miliki zaidi ni baadhi tu ya ile Miradi ambayo Rais amepigia upato wa mafanikio ya Serikali yake.

Pia ametaja ufunguzi wa Bandari ya Lamu na ile ya Kisumu kama kigezo cha uchumi. Amesema kuwa anatarajia biashara baina ya Serikali ya Kenya na nchi jirani zitaimarika zaidi.

Pia Rais Kenyatta amewataka viongozi kutoendeleza siasa za kuwagawanya Wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *