• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Uhuru Aamrisha Uchunguzi Ufanywe Baada ya Mwanamazingira Kuuawa

Jul 16, 2021
257 300

Rais Uhuru Kenyatta ameshtumu mauaji ya mhifadhi wa mazingira Bi Joanna Stuchburry na kuamrisha Vitengo vya usalama kuwasaka wahusika wa kitendo hicho cha ukatili.

Bi Stuchburry, anayejulikana kutokana na juhudi zake thabiti za kuhifadhi msitu wa Kiambu, aliuawa na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi nyumbani kwake siku ya Alhamisi mchana.


Kwenye ujumbe wake wa rambirambi kwa familia, jamaa na marafiki, Rais Kenyatta alisema serikali yake inatambua pakubwa mchango wa Bi Stuchburry katika uhifadhi wa mazingira.


“Ni huzuni, bahati mbaya na masikitiko kwamba watu wabaya wamemuua Bi Joanna Stuchburry katika hali hiyo ya kikatili.


“Kwa muda mrefu, Bi Joanna amekuwa mtetezi imara wa uhifadhi wa mazingira na anakumbukwa kutokana na juhudi zake thabiti za kulinda msitu wa Kiambu dhidi ya kunyakuliwa,” Rais aliomboleza.


Aidha ameahidi hatua za serikali kuwasaka na kuwatia mbaroni wauaji wa Bi Stuchburry na kuwataja kuwa maadui waoga wa taifa.


“Serikali yangu itawasaka na kuwatia mbaroni wahalifu waliotekeleza mauaji ya Bi Joanna. Hatutaruhusu watu wachache binafsi kuendelea kumwaga damu ya watu wasio na hatia ambao wanafanya bidii kuiboresha Kenya kwa manufaa ya sisi sote. Hao ni maadui waoga wa nchi yetu,” alisema Rais Kenyatta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *