• Thu. Jun 20th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Uhesabu wa kura wasitishwa Kiambaa

Jul 16, 2021
304 300

Shughuli za uhesabu Kura katika eneo la Kiambaa umesitishwa kwa Muda baada ya Mgombeaji wa Jubilee Kariri Njama kulalamikia dosari katika vituo vitatu akitaka uhesabu urejelewe.


Vurugu zilishuhudiwa katika shule ya Upili ya Karuri ambako shughuli za uhesabu Kura katika uchaguzi mdogo uliokamilika kiambaa unaendelea.

Kabla ya shughuli nzima kisitishwa Mgombeaji wa Chama Cha UDA Wanjiku John alikuwa anaongoza kwa kura 21,301 akifuatiwa kwa karibu na yule wa Jubilee Kariri Njama na Kura 21,057 baada ya vituo 152 kuhesabiwa kati ya vituo154.


“Unaona, walikuwa wametangaza matukio mapema wakasema Wanjiku alikuwa na kura 21, 301 na Mimi 21,057, kwenda kuangalia tena tunapata Wanjiku ameongezewa kura, hizi kura wametoa wapi, afisa huyu anayetangaza kura anatuhadaa,”Kariri alisema mapema leo.


Mwendo wa saa kumi na Mbili asubuhi, afisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Peter Mwigai alikiri Pana tashwishi katika uhesabu huo na akatangaza kusimamishwa kwa Muda.


Aidha wanasiasa wanaoegemea mrengo wa Tangatanga wakiongozwa na Seneta Murkomen na wengineo, walikuwa tayari washaanza Kusherehekea kwenye mitandao kwa kumpongeza Wanjiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *