• Tue. Oct 8th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Uchaguzi wa Uasu Watolewa Kisumu Kwa Hofu ya Corona

Jun 17, 2021
307 300

Wahadhiri wakiongoozwa na afisi ya sasa imeendeleza kampeni zake sehemu za Nyanza kwa matayarisho kikamilifu kufikia tarehe 23 mwezi huu yaani wiki ijayo.

Uchaguzi wa kitaifa katika Chama cha wahadhiri UASU sasa umeondolewa kule Tom Mboya College Kisumu na sasa utafanyika  Nakuru .

Kulingana na Onesmus Mutio  kutoka chama hicho wamechukua hatua hiyo kuzuia makali ya Corona Kisumu huku pia wakitaka wa kuwalinda wahadhiri waachama wao watakaoshiriki katika uchaguzi huo dhidi ya makali ya homa hiyo.

‘‘Tumekuwa na mkutano wa baraza kuu la chama na tumeamua kuandaa uchaguzi hapa Nakuru kwa sababu ya ongezeko la ugonjwa wa Corona mji wa Kisumu kwani ni yetu kubwa ni kuhakikisha kuwa tumewalinda pia wahadhiri wetu.’’ Alisema Mutio.

Kundi  hili ni Muga Kolale anayewania uenyekiti,Constantine Wasonga katibu mkuu na Onesmus ambaye anawania kiti cha mratibu mkuu wa kitaifa.

‘‘Tumetembea maeno Kadhaa tukiomba kura na sasa tuko sehemu za Nyanza tukiuza sera zetu ,ajenda yetu ya kwanza tukiingia afisini ni kuhakikisha kuwa tumefufua bim aya afya ya wahadhiri.’’ Alidokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *